Saturday, September 6, 2014

HALI YA NANE NANE 
2014.
Kwa hali ya kawaida maonesho ya Nane Nane katika Taifa letu hili yanaashiria changamoto nyingi hususani kwa Wakulima na Wafugaji kwasababu walio wengi ambao wanatembelea sehemu husika wanabadilishana maarifa katika kada mbili hizi kwani wafugaji wanapata kitu kutoka kwa wakulima na wanahamasika kwa hali ya juu sana, pia wakulima nao wanapata maarifa kutoka kwa wafugaji na uelewa unaongezeka sana.
Kwa mtu yeyote aliyetembelea au ambaye anapenda kutembelea maonesho haya atakiri kuwa ni kweli kabisa sababu kuna watu wanahamasishwa kulima na wengine kufuga, nyanja zote hizi mbili ni kitu muhimu kwa binadamu kwani huweza kumfanya mtu aweze kuishi kwasababu binadamu yeyote yule anastahili kula na chakula hicho kinapatikana katika maeneo haya mawili (ufugaji na ukulima).
Bustani ya mboga mbali mbali
Nyanya zilizostawi vizuri


Nikitathimini uoteshaji wa mazao mbali mbali husani Nyanya ndani ya Green House katika viwanja vya John Mwakangale (Nane nane Mbeya 2014)

Napenda kuwashawishi watu walio wengi kulima na kufuga kwa hali na mali kwani Kilimo sasa ni biashara na sio kulima kwa mazoea tu. Tujitahidi kwa kuweza kujikita katika nyanja mbili hizi. Ahsanteni

No comments:

Habari ya majukumu wadau, Niwapongeze kwa kuendelea kupambana na majukumu mbalimbali katika kuendeleza shughuli za kilimo na mifugo, nawapo...